Message Us

AZANIA BANK LAUNCHES AMSHA NDOTO SAVING CULTURE CAMPAIGN

Azania Bank Launched a saving culture campaign on 27th June 2019 to convince and entice Tanzanians to save more to be financially independent.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Benki ya Azania yazindua Kampeni Ya ‘AMSHA NDOTO’ kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa Watanzania.

Dar-es-salaam, Juni 27, 2019: Benki ya Azania (ABL) leo imetangaza uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina, ‘Amsha Ndoto’ yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.


Kampeni itaendeshwa kwa miezi mitatu, kuanzia 27 Juni 2019 hadi 27 Septemba 2019 na itahusisha wateja wa zamani na wapya ikijikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti na Watoto Akaunti.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa ABL, Charles Itembe, kutakuwa na zawadi nyingi kwa washindi ambao watakuwa na vigezo vya kushiriki katika promosheni ya kampeni hii ambapo watapokea zawadi zitakazowasaidia kufikia malengo na ndoto zao.
Akiongelea kuhusu vigezo vya washiriki, Itembe alisema kuwa wateja ni lazima waweke akiba ya kiasi cha TZS 500,000 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima, na wale watakaoweka akiba kiasi cha TZ 1,000,000 watapewa tokeni zitakazowawezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho itakayowapata washindi.
“Tunawahamasisha wazazi wote na walezi kuwafungulia Watoto wao ‘Watoto Akaunti’ ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye”, alisema Itembe, akigusia pia kuwa Watoto Akaunti inakuwa kama msingi wa kuwaandaa watoto kujifunza namna ya kuweka akiba kuanzia kwenye umri mdogo.


Promosheni hii, yenye kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde,tumuwezeshe ada ya shule’, itawasilishwa kupitia radio na mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn, Google Display placement na tovuti za ndani. ABL pia imetengeneza tovuti ndogo kwa wateja wapya kujiunga na inaweza kupatikana kupitia linki hii: amshandoto.com.
Masharti na vigezo kuzingatiwa


News Link: https://www.ippmedia.com/sw/biashara/%E2%80%98amsha-ndoto%E2%80%99-kuhamasisha-uwekaji-akiba

- 15 Aug 2019 10:01:06